Mtakatifu Patriarki wa Mosko na Rusi Yote Kirill (uraiani – Vladimir Mikhailovich Gundyaev) alizaliwa tarehe 20 Novemba, 1946 jijini Leningrad.
Baba mzazi – Mikhail Vasilyevich Gundyaev, padri, alifariki mwaka 1974.
Mama mzazi – Raisa Vladimirovna Gundyaeva, mwalimu wa lugha ya Kijerumani shuleni, katika miaka ya mwisho-mwisho alikuwa mama wa nyumbani, na alifariki mwaka 1984.
Kaka mkubwa – Paroko Nikolai Gundyaev, Profesa katika Chuo cha Theolojia cha St. Petersburg, Msimamizi wa heshima wa Kanisa Kuu la Utakaso lililoko St. Petersburg.
Babu – Padri Vasily Stepanovich Gundyaev, mfungwa wa Solovki, ambaye alifungwa na kupelekwa uhamishoni kutokana na shughuli zake za kikanisa na mapambano dhidi ya mageuzi katika miaka ya 20, 30 na40 ya karne ya ishirini, makosa ambayo hukumu yake ilikuw nikwenda jela na pia kupelekwa uhamishoni.
Baada ya kuhitimu masomo ya darasa la 8, Vladimir Gundyaev aliajiriwa katika Msafara wa utafiti wa kijiolojia wa Leningrad, wa Idara ya Jiolojia Kanda ya Kaskazini-Magharibi, ambako alifanya kazi kuanzia mwaka 1962 hadi 1965 kama fundi-mchora ramani, akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya sekondari.
Baada ya kuhitimu shule ya sekondari mnamo mwaka 1965, alijiunga na Seminari ya Theolojia ya Leningrad, na kisha Chuo cha Theolojia cha Leningrad, ambako alihitimu kwa ufaulu wa juu mnamo mwaka 1970.
Tarehe 3 Aprili, 1969 alipakwa mafuta ya utawa na Mitropoliti Nikodim (Rotov) wa Leningrad na Novgorod, na akapewa jina la Kirill.
Mnamo tarehe 7 Aprili, aliwekewa mikono na kuwa Dekani, ambapo tarehe 1 Juni ya mwaka huo huo akawa Dekani – Kiongozi.
Tangu mwaka 1970 – Mtheolojia-mteule katika Chuo cha Theolojia cha Leningrad.
1970-1971 – Mwalimu wa Theolojia na Msaidizi wa Mkaguzi wa Shule za Theolojia za Leningrad; wakati huo huo akiwa katibu-mahsusi wa Mitropoliti Nikodim wa Leningrad na Novgorod, na mkufunzi-daraja la 1
wa seminari.
Tarehe 12 Septemba, 1971, alipandishwa cheo na kuwa Padri-kiongozi.
Miaka 1971-1974 – Mwakilishi wa Patriarkia ya Mosko katika Baraza la Makanisa Ulimwenguni kule Jeneva.
Kuanzia tarehe 26 Desemba, 1974 hadi tarehe 26 Desemba, 1984 – Mkuu wa Chuo cha Theolojia cha Leningrad.
Miaka 1974-1984 – Profesa-Mshiriki wa Idara ya Patrolojia ya Chuo cha Theolojia cha Leningrad.
Tarehe 14 Machi, 1976, aliwekwa wakfu kuwa Askofu wa Vyborg.
Tarehe 2 Septemba, 1977, alipandishwa cheo na kuwa Askofu Mkuu.
Kuanzia tarehe 26 Desemba, 1984 – Askofu Mkuu wa Smolensk na Vyazma.
Tangu mwaka 1986, amekuwa akisimamia parokia katika mkoa wa Kaliningrad.
Tangu 1988 —- Askofu Mkuu wa Smolensk na Kaliningrad.
Kuanzia Novemba 13, 1989 hadi 2009 – Mwenyekiti wa Idara ya Mahusiano ya Kikanisa na nchi za Nje (tangu Agosti 2000 – Idara ya Mawasiliano ya Kikanisa na nchi za Nje), mwanachama wa kudumu wa
Sinodi Takatifu.
Tarehe 25 Februari, 1991 alipandishwa cheo na kuwa Mitropoliti.
Huku akitimiza utiifu wa kikuhani, Mtakatifu Kirill alikuwa:
Tangu 1975 hadi 1982 – Mwenyekiti wa Baraza la Dayosisi la Mitropolia ya Leningrad;
Kuanzia 1975 hadi 1998 – Mjumbe wa Kamati Kuu na Kamati-Tendaji ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni;
Tangu 1976 hadi 1978 – Naibu Patriarki wa Esarkia ya Ulaya Magharibi;
Kuanzia 1976 hadi 1984 – Mjumbe wa Tume ya Sinodi Takatifu ya Umoja wa Wakristo;
Kutoka 1978 hadi 1984 – Msimamizi wa Parokia za Patriarkia nchini Finland;
Kuanzia 1978 hadi 1984 – Naibu Mwenyekiti wa tawi la Idara ya Mahusiano ya Kikanisa na nchi za Nje mjini Leningrad;
Tangu mwaka 1980 hadi 1988 – mjumbe wa tume ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 1000 ya Ubatizo katika Rusi;
Mnamo mwaka 1990 – akawa mjumbe wa tume ya maandalizi ya Baraza la Mitaa la Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi;
Mwaka 1990 – mjumbe wa tume ya kusaidia juhudi za kudhibiti madhara yaliyotokana na ajali ya Chernobil;
Tangu mwaka 1989 hadi 1996 – Kiongozi-Mtendaji wa Dekania ya Kiorthodoksi ya Hangari;
Kuanzia mwaka 1990 hadi 1991 – Kiongozi wa Muda wa Dayosisi ya Hegi-Uholanzi;
Tangu mwaka 1990 hadi 1993 – Kiongozi wa muda wa Dayosisi ya Korsun;
Kuanzia mwaka1990 hadi 1993 – Mwenyekiti wa Tume ya Sinodi Takatifu ya kufufua elimu, mapendo na maadili ya kidini;
Kuanzia mwaka 1990 hadi 2000 – Mwenyekiti wa Tume ya Sinodi Takatifu ya kufanya marekebisho ya Mwongozo wa Uendeshaji wa Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi. Mwongozo huu ulipitishwa katika kikao cha Baraza la Maaskofu la Yubilei mwaka 2000;
Kutoka mwaka 1994 hadi 2002 – Mjumbe wa Baraza la Jumuiya ya Uamsho wa Kanisa Kuu la Kristo Mwokozi jijini Mosko;
Kuanzia mwaka 1994 hadi 1996 – Mjumbe wa Baraza la Sera ya Mambo ya Nje ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi;
Kuanzia mwaka 1995 hadi 2000 – Mwenyekiti wa Kikosi-Kazi cha Sinodi kwa ajili ya kuandaa dhana ya Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi juu ya maswala ya mahusiano kati ya Kanisa na serikali, pamoja na changamoto za jamii ya leo kwa ujumla.
Kutoka mwaka 1995 hadi 1999 – Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi na utekelezaji wa maadhimisho ya tarehe-kumbukizi za Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1941-1945);
Kutoka mwaka 1996 hadi 2000 – Mjumbe wa Bodi ya Usimamizi wa Mfuko wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Ushindi.
Tarehe 27 Januari, 2009, Baraza Kuu la Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi lilimchagua Mitropoliti Kirill kuwa Patriarki wa Mosko na Rusi Yote.
Tarehe 1 Februari, 2009 Mtakatifu Patriarki Kirill alisimikwa rasmi.