Metropolitani Leonid: Matukio nchini Ukraina yana athari hasi kwa misheni ya kibinadamu barani Afrika - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ

Metropolitani Leonid: Matukio nchini Ukraina yana athari hasi kwa misheni ya kibinadamu barani Afrika

Matukio ya Ukraina na vikwazo dhidi ya Urusi vina athari hasi kwa utume wa kibinadamu wa Kanisa la Kiothodoksi la Urusi barani Afrika. Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Afrika, Metropolitani wa Klin Leonid, katika mahojiano na mwandishi wa TASS mnamo Desemba 19, 2022.

“Mtakatifu Patriarka Kirill na Rais wa Urusi Vladimir Putin wameongea  mara kadhaa kuhusu hili. Tuko katika hatua za mwanzo katika kusaidia nchi zenye mahitaji maalum, na hizi, kwanza kabisa, ni nchi za Kiafrika,” kiongozi huyo alibainisha.

“Tunaongea juu ya usambazaji wa nafaka, mbolea, ambazo tumekusanya tani elfu 150 na zimelundikana katika bandari za Ulaya. Na hawa  wazungu “waliostaarabika” hawairuhusu Urusi kuchukua mbolea hii na kuitoa kwa Afrika,” Metropolitani Leonid aliongeza.

“Vivyo hivyo kwa mpango wa nafaka. Tumefanya makubaliano yote, lakini nchi zinazohitaji chakula haziwezi kupata nafaka kutoka kwetu. Bila shaka, hili ni suala ambalo uongozi wa kisiasa wa Urusi unalishughulikia, lakini Kanisa pia linashiriki katika hili kwa kupeleka misaada midogo-midogo ya kibinadamu. Tunanunua nafaka kwa fedha zilizotolewa na waumini wetu, mfuko wa “panda mbegu”, – vyanzo hivi vinatuwezesha kutoa msaada wa kibinadamu kwa maelfu ya watu katika nchi maskini zaidi za Afrika,” Askofu Mkuu alisema.

“Ukraina ni mada nyeti sana, ni bora kuwasiliana na wawakilishi wa Idara ya Mahusiano ya Kikanisa na Nchi za Nje juu ya suala hili. Lakini kwa niaba yangu mwenyewe, naweza kusema: Kanisa la Kiothodoksi la Ukraina ndilo Kanisa pekee ambalo leo kikanuni lina haki – fulani kivyake, kwa sababu “Kanisa la Kiothodoksi la Ukraina” ni kundi lenye mifarakano,” Metropolitani Leonid alisisitiza. “OCU”, kikundi cha watu kilichoundwa kwa njia za ulaghai, na ambacho kilipatiwa “tomos” na Patriarka Batholomayo; ni muundo usio na neema wala baraka za kikanuni.”

“Kwa bahati mbaya, hivi sasa hatusikii taarifa za kufurahisha kutoka kwa uongozi wa Kanisa la Kiothodoksi la Ukraina. Kwa mfano, kwamba wameacha kumwadhimisha Mtakatifu Patriarka Kirill, kwamba kwa maamuzi ya upande mmoja wamejiondoa kwenye (masharti) ya katiba, ambayo ilitolewa katika muda wake, na Patriarka wa Mosko na Urusi Yote (Aleksei wa Pili). Sinodi ya Kanisa la Kiothodoksi la Urusi itatoa tathmini yake kamili, lakini tunaelewa, bila shaka, kwamba watu wa Ukraina kwa kiasi fulani wako chini ya shinikizo kali la kisaikolojia na la kimwili kutoka kwa mamlaka za nchi yao,” Askofu alisema.

“Kila Kanisa la Eneo linachukuliwa kuwa ni Kanisa ambalo linaweza kujiamulia mambo yake lenyewe na kujiongoza kwa kujitegemea. Wana Sinodi zao, ambazo huleta masuala mbali mbali, mazito, katika ajenda ya kimataifa ili kuidhinishwa,” Askofu Mkuu alibainisha.

“Zaidi sana sasa, kuliko kipindi chochote kile, ni lazima maamuzi yote tufanye kwa pamoja. Muundo wa Kiothodoksi wa Ulimwengu  haumaanishi ukuu wa Kanisa moja la Eneo kuwa juu ya lingine. Ikiwa baadhi ya masuala ya kimataifa yanahitaji mabadiliko katika ajenda ya kimataifa, basi kuna mikutano kati ya Waothodoksi, mikutano ya mabaraza kwa ajili ya hili. Maamuzi yote kuhusu Uothodoksi  Ulimwenguni yanapaswa kuamuliwa na Makanisa ya Kiothodoksi ya Maeneo,” alisisitiza Askofu Mkuu.

“Hakuna hata Patriarka mmoja aliye na haki ya kuamua, peke yake, maswala ya Kiothodoksi, kama aonavyo, jinsi anapaswa kutenda katika hali hii au ile na kisha kumweka kila mtu mbele ya ukweli,” Metropolitani Leonid alijumuisha. “Hii inasababisha mgawanyiko, na matukio ya kutisha ambayo tunashuhudia

Shirikisha katika mitandao ya kijamii: