Metropolitani wa Klin Leonid Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika - Esarkia ya Kipatriarki ya Afrika
RUS | ENG | FRA | SWA | DEU | عرب | Ελλ | PT
Tovuti rasmi
Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika

Metropolitani wa Klin Leonid Askofu Mkuu wa Esarkia ya Afrika

Alizaliwa tarehe 26 Oktoba 1968 katika mji wa Stavropol.

Mwaka 1985 alihitimu kutoka shule ya sekondari, ambapo mwaka 1985-1986 alifanya kazi kama mhudumu katika maabara ya  Idara ya “Aerodynamics and Flight Dynamics”. Wakati huo huo, akipata mafundisho ya mimbari katika Kanisa la  Mtakatifu George la mjini Krasnodar.

Kati ya mwaka 1986 na 1988 alitumikia Jeshi la Ulinzi.

Mwaka 1988-1989 alikuwa shemasi-msaidizi wa Askofu Mkuu wa Isidore ya Ekaterinodar na Kuban.

Katika miaka ya 1989-1992 alisoma katika Seminari ya Kiroho jijini Leningrad.

Tarehe 8 Aprili, 1990, aliwekewa mikono kuwa Shemasi.

Tarehe 18 Juni, 1990, aliwekwa wakfu kuwa  Mtawa .

Tarehe 8 Oktoba, 1990, aliwekewa mikono kuwa  Padri.

Katika miaka ya 1990-1997, alikuwa Kasisi wa Kanisa Kuu la Ekaterinodar katika mji wa Krasnodar. Katika miaka ya 1995-1997, Msimamizi wa Kanisa.

Mwaka 1997 alihamishiwa Mosko ili kufanyakazi katika Idara ya Sinod inayofanya kazi pamoja na vikosi vya Jeshi la Ulinzi na taasisi za kusimamia sheria.

Kuanzia Machi hadi Septemba 1998, alikuwa katika kundi la huduma katika kikosi cha askari – wa – miavuli, cha brigedi ya kulinda amani nchini Bosnia na Herzegovina.

Kuanzia Oktoba 1998 hadi Septemba 2002 alisoma katika Kitivo cha Theolojia cha Chuo Kikuu cha Athens, na alikuwa Kasisi-msaidizi wa hekalu-dogo la Kirusi, la Mtakatifu Panteleimon, Aharnon (Athens, Ugiriki).

Tangu Oktoba 2002- Mfanyakazi wa Sekretarieti ya Mahusiano ya Kimataifa ya Idara ya Mambo ya Nje, ya Patiarkia ya Mosko. Alifanya safari fupi –fupi za kimisioni katika maeneo ya  Athos, Finland na India.

Kuanzia Mei 2003 hadi Desemba 2004–Mfanyakazi katika Misioni ya Kiroho mjini Yerusalemu.

Kwa azimio la Sinodi Takatifu, Desemba 2004  aliteuliwa kuwa Mwakilishi wa Patriarki wa Mosko na Urusi yote, katika Patriarkia ya Aleksandria na Afrika yote.

Tarehe  11 Aprili, 2010, katika boma la Patriarkia ya Mosko mjini Cairo, Mtakatifu Kirill Patriarki wa Mosko na Urusi yote, alimsimika kuwa “Archimandrite”.

Kwa azimio la Sinodi Takatifu, la tarehe 29 Mei, 2013, alichaguliwa kuwa Askofu wa Argentina na Amerika ya Kusini.

Tarehe 11 Juni, katika Kanisa la Watakatifu Wote, alisimikwa kuwa Askofu – Mkazi katika Monasteri ya Danilov mjini Mosko.

Tarehe 17 Juni, kwa Liturgia takatifu, aliwekwa Wakfu katika kanisa la Mtakatifu Igor Chernigovsky.

Kwa azimio la Sinodi takatifu, la tarehe 3 Juni, 2016, aliteuliwa kuwa Askofu wa Vladikavkazky na Alansky.

Kwa azimio la Sinodi takatifu, la tarehe 27 Desemba, 2016, aliteuliwa kuwa Patriarki-Kiongozi wa  parokia za Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi katika Jamhuri ya Armenia, huku akiendelea kuongoza  Dayosisi ya Vladikavkaz.

Tarehe  4 Desemba, 2017, kwa Liturgia takatifu, ;katika Kanisa Kuu la Kristo Mwokozi, la Mjini Mosko, alisimikwa na Mtakatifu Patriarki Kirill, kuwa Askofu Mkuu.

Kwa amizio la Sinodi Takatifu, la tarehe 17 Oktoba, 2019, aliteuliwa kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Idara ya Mahusiano ya Nje, huku akiendelea kuiongoza  dayosisi ya Vladikavkaz.

Kwa azimio la Sinodi Takatifu, la tarehe 29 Oktoba, 2019, aliteuliwa kuwa Mwenyekiti-Mwenza wa Kikosi- Kazi cha kuratibu ushirikiano kati ya Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi na Kanisa la Malankara.

Kwa azimo la Sinodi Takatifu, la tarehe 11 Machi, 2020, aliteuliwa  kuwa Mwenyekiti-Mwenza wa Tume ya Mazungumzo kati ya Kanisa la Kiorthodoksi laUrusi na Kanisa la Ethiopia.

Kwa azimio la Sinodi Takatifu, la tarehe  24 Septemba, 2021, aliondolewa usimamizi wa Dayosisi ya Vladikavkaz, ila akabakizwa  katika nafasi ya Kaimu Mwenyekiti wa DECR na Patriarki-Kiongozi wa kanisa la Armenia, na akateuliwa kuwa  kasisi wa Patriarkia Kuu ya Mosko na Urusi yote,  akapewa cheo cha “Klinsky”, na kibali cha kuweka makazi mjini Mosko..

Kwa agizo la Mtakatifu Kirill Patriarki wa Mosko na Urusi yote, la tarehe 11 Oktoba, 2021,aliteuliwa kuwa Kasisi-Kiongozi wa Nyumba ya Watawa ya Patriarkia ya Mosko na Urusi yote , ya Kanisa la Watakatifu Wote  katika Kulishki za jiji la  Mosko.

Kwa azimio la Sinodi takatifu, la tarehe 15 Oktoba, 2021, aliteuliwa kuwa Askofu wa Erevan na Armenia, na kuendelea na wadhifa wa Kaimu Mwenyekiti wa DECR.

Kwa azimio la Sinodi Mtakatifu, la 29 Desemba, 2021, aliteuliwa kuwa Patriarki Klinsky, Patriarki wa Esarkia ya Afrika na akapewa jukumu la kuongoza dayosisi za  Afrika ya Kakazini, na pia kukaimu uongozi wa dayosisi za Afrika ya Kusini. Aliondolewa majukumu ya Kukaimu Uenyekiti wa DECR, ila akabakiziwa uongozi wa Daypsisi za Erevan-Armenia.

Desemba 2021, alifaulu mtihani wa shahada ya “Master’s” kwa kuwasilisha mada ya “Haki za kimataifa katika kuwalinda Wakristo wachache walioko Mashariki ya Kati na Afrika – Kaskazini” (katika Chuo Kikuu cha Urafiki wa Mataifa, cha Urusi – Kitengo cha Sheria, Idara ya Sheria za Kimataifa).

Tarehe 7 Januari, 2022, katika ibada ya jioni ya Kanisa Kuu la Kristo Mwokozi lililoko Mosko, Mtakatifu Kirill, Patriarki wa Mosko na Urusi yote, alimsimika Askofu Klinsky Leonid kuwa Mtakatifu Mitropolit.